Wanachama wa kundi la ulinzi wa jamii la Zairr, wamejisalimisha kwa jeshi la Kongo na kusaini muafaka wa amani wa upande mmoja, katika eneo lenye machafuko la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa kundi hilo, Jean-Marie Ngadjole amesema wapo tayari kujiunga na mchakato wa amani na kushiriki katika mpango wa utangamano wa jamii, utakaoongozwa na mamlaka za Kongo.
Aidha, kundi hilo lenye sehemu kubwa ya Vijana, liliwasili katika mji mkuu wa mkoa huo, Bunia wakitumia usafiri wa magari kadhaa wakiwa wamevalia nguo za kiraia bila ya kuwa na silaha.
Sehemu ya kundi la ulinzi lililoundwa mwaka wa 2019 kuyalinda maslahi ya jamii tano ambazo zimekuwa waathiriwa wa ukatili unaofanywa katika mkoa wa Ituri karibu na mpaka na Uganda.