Mkaguzi Kata wa Kata ya Ngulyati, iliyopo Bariadi Mkoani Simiyu, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Robert Mtula ameonya tabia ya Vikundi vya ulinzi Shirikishi kutoa adhabu kwa Wananchi majira ya usiku, wakati wakitekeleza majukumu yao kwani ni kinyume na matakwa ya Sheria, kanuni na taratibu.
Mkaguzi huyo ameyasema hayo hii leo Januari 30, 2024 wakati alipotembelea kikundi cha Ulinzi Shirikishi cha Nyasosi, kilichopo Kata ya Ngulyati Wilaya ya Bariadi.
Aidha, amewakumbusha kuhusu wajibu wao wakati wanapotekeleza majukumu mbalimbali, kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya kihalifu na kuwafikisha watuhumiwa vituo vya Polisi.