Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero, Mrakibu wa Polisi, Daudi Nkuba kwa kushirikiana na wanakamati wa sherehe ya siku ya familia ya  Polisi (Police Family Day) wamehitimisha sherehe hizo kwa kufanya matendo ya huruma ambapo Januari 28, 2024 wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya Mtakatifu Francis iliyopo Ifakara mjini.

Akizungumza na Dar24 Media mara baada ya kutoa misaada hiyo OCD Nkuba amesema licha ya kusherekea sherehe ya Polisi ya kufunga na kufungua mwaka 2024 lakini wameona sherehe yao haitakuwa ya baraka kama hawata ikamilisha na matendo ya huruma na kuchagua kutembelea hospitali hili kuwapa mahitaji mbalimbali wagonjwa na wazazi.

Anna Daudi Mama aliejifungua watoto mapacha, amefarijika kujifungua siku hiyo kwani mbali ya kuwa ni siku ya familia ya Polisi lakini pia ilikuwa ni siku ya kuzaliwa Rais Samia Hassan Suluhu, hivyo amewashukuru na kusema zawadi alizozipata zitasaidia kwani alijiandaa kwa mtoto mmoja, ila amejifungua mapacha.

Lengo la sherehe ya siku ya familia ya Polisi (Police Family Day) ni kukutana hili kufurahi kwa pamoja,  kubadilisha uzoefu, kufahamiana na kushirikiana kwenye mambo mbalimbali.

Hassan Shehata: Timu ya Misri akabidhiwe mzawa
Kocha Morocco akubali lawama AFCON 2023