Kocha wa timu ya Taifa ya wasichana wenye umri chini ya umri miaka 17 ‘Serengeti Girls’, Bakari Shime, amesema amekiandaa kikosi chake kuanza kwa kishindo mechi za kujiandaa kufuzu Kombe la Dunia.

Serengeti Girls itaanza kampeni za kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa kujuliza kwa Zambia katika mechi ya awali itakayopigwa Jumamosi jijini Lusaka, Zambia.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Shime amesema timu inaendelea kufanya mazoezi kwa bidii na ipo tayari kwa mchezo.

Shime alisema vango ya wachezaji wake vimeimarika kwa aslimia kubwa, wana ari ya mchezo na anaamini watapambara na kupata matokeo mazuri

“Timu ipo tayari kuanza mapambano ya kuwania nafasi ya kufuzu, nina kikosi bora ambacho kinajua umuhimu wa kufanya vyema katika mchezo ujao na mingine itakayofuata kwa lengo la kufuzu” amesema Shime.

Ameongeza kuwa atahakikisha anaiongoza Serengeti Girls kupata matokeo mazuri na kuruda rekodi iliyowekwa mwaka juzi ya kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Tanzania inatafuta tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia baada ya kushiriki fainali za mara ya kwanza zilizofanyika mwaka 2022 nchini India.

Katika fainali hizo, Tanzania ilipambana na kuiishia hatua ya robo fainali.

Polisi yafafanua tukio Baba, Mtoto kupotea
Wanaowatumia Watoto kusafirisha Dawa za kulevya waonywa