Bertina Mangosongo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh amesema jumla ya wagonjwa 4,579 wa ugonjwa wa macho (Red Eyes) wameripotiwa katika vituo vya afya, na Hospitali na kwamba idadi ya takwimu hizo zimejumuisha wagonjwa waliofika kwenye vituo vya afya na Hospitali za binafsi na Serikali Unguja na Pemba.

Hafidh ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, huku akiwataka wananchi kuacha kutumia dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo, ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza sambamba na kuchukua tahadhari za usafi ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara ili kujikinga na maradhi hayo .

Amesema, endapo jamii itaendelea kutumia dawa hizo kunaweza kuongeza ukubwa wa tatizo hilo hivyo aliwataka wananchi kufika hospitali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa huo ili kupata matibabu stahiki na kwa wakati sahihi huku akiitaka jamii kutumia maji baridi kunawia uso mara kwa mara na kujitenga wakati wa kusubiri huduma katika vituo vya afya, ili kuepusha maambukizi mapya.

“Ni vizuri mgojwa yeyote wa macho asisubiri eneo walilokaa wagonjwa wengine atibiwe chumba maalum kilichotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa namna hiyo na akimaliza matibabu aende moja kwa moja nyumbani ili kupunguza hatari ya maambukizi mapya”alisema naibu Waziri,” alisema.

Awali, akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusiana na ugonjwa huo, Mratibu wa Huduma za Afya ya Msingi na Matibabu ya Macho, Dkt. Rajab Mohammed Hilal amesema ugonjwa wa macho mekundu husababishwa na virusi wanaoitwa Adenovirus na kupelekea maambukizi ya kirusi kwenye ngozi nyembamba inayozunguka gololi la jicho (conjunctiva) pamoja na kioo (Cornea) cha jicho.

 

Makamba anadi fursa Biashara, Uwekezaji Italia
Sopu, Akaminko watajwa Simba SC