Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, imetoa onyo kwa wote wanaotumiwa kusafirisha na watumiaji wa Dawa za kulevya kwani wanayo orodha yote ya Watoto wanao shiriki kuuza Dawa hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo amesema pia hivi karibuni wataanza msako mkali wa kufuatilia kumbi zote za starehe na Hoteli kukagua shisha zilizo changanywa na Dawa ya kulevya.

Amesema, “Takwimu za Watoto ambao wanaingizwa kwenye usafirishaji wa madawa ya kulevya tunazo na siku si nyingi tutawaunganisha wale wote wanaotumiwa kuuza madawa ya kulevya.”

Aidha, Kamishna Lyimo ameongeza kuwa, “tunaomba wazazi na walezi kuwalinda watoto wetu kuepuka na madawa ya kulevya kwasababu yapo makundi ambayo yanatumiwa na watumiaji wa madawa hayo,unakuta mtoto anaenda shule anaishia njiani na kubana kwenye vichochoro ambavyo wapo watumiaji wa madawa.”

 

Serengeti Girls mguu sawa Zambia
Uhalifu: Jaji Mkuu aibua hoja kuukabili uhalifu nchini