Watu wasiojulikana, wameiba majeneza mawili na mabati 10 katika Msikiti wa Marhaba ulioko Bakarani mjini Mombasa Nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Mzee wa mtaa huo, Mohamed Hamid amesema waligundua kutoweka kwa majeneza hayo mawili yaliyotengenezwa kwa chuma, wakati walipotaka kubebea maiti zilizofikishwa msikitini kuswaliwa.

Amesema, kufuatia tukio hilo wanapanga kufanya maombi maalum ‘albadiri’, ili kulaani waliohusika na wizi huo wanaosema sio wa kawaida uliofanyika katika Msikiti huo uitwao Masjid Mar-haba.

Hata hivyo, taarifa ya Polisi wa Kituo cha Kisauni Mombasa imeeleza kuwa maafisa wake wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu hao na kuwachukulia hatua.

Krepin Diatta asubiri kitanzi CAF
Maafande waiandalia dozi Young Africans