Hatimaye Uongozi wa Simba SC umetangaza kumsamehe Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chama, baada ya kumsimamisha kwa mwezi mmoja na nusu.

Kiungo huyo alisimamishwa klabuni hapo mwezi Desemba mwaka jana (2023), kwa tuhuma za utovu wa nidhamu anaodaiwa kuufanya kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Simba SC imetangaza kumsamehe Chama, kupitia taarifa maalum iliyochapishwa katika vyanzo vya klabu hiyo mapema leo Ijumaa (Februari 02).

Taarifa hiyo imeeleza: Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu Wanachama na Wapenzi wa Simba kuwa umemsamehe mchezaji Clotous Chama.

Hatua hii imefuatia maamuzi ya Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Simba ambayo ilipitia barua ya maelezo ya chama na pia uamuzi wa kocha Benchica wa kumsamehe chama, hivyo Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Simba ikaridhia kumsamehe na kusitisha kumfikisha kwenye Kamati ya maadili ya Klabu ya Simba.

Chama anaungana na Kikosi cha Sinba kilicho Mkoani Kigoma kwa mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Klabu ya Simba itaendela kutilia mkazo ustawi wa nidhamu kama nguzo muhinmu ya kujenga timu imara. Nidhanu ni moja ya tunu (values) za kiabu ya Simba.

Matola: Fanyeni subra mtafurahi
AFCON 2023 - Vumbi la Robo Fainali kutimka