Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos amewaambia wachezaji wake kuwa “sasa wafikirie kuhusu kucheza fainali” baada ya ushindi wa hatua ya 16 bora dhidi ya Morocco iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Evidence Makgopa na Teboho Mokoena walifunga katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco iliyocheza Nusu Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Bafana Bafana sasa itakutana na Cape Verde katika mchezo wa Robo Fainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika kesho Jumamosi (Februari 03), ambapo ilianza kampeni zake kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Mali, lakini walifuzu kwa hatua ya 16 bora katika kundi ambalo lilishuhudia mabingwa wa mwaka 2004 Tunisia wakitolewa.

“Kitu muhimu sana ni kuwa unaweza kusonga mbele katika mashindano, unapokuwa bora,” amesema Broos.

“Ni jambo zuri sana katika mashindano haya Afrika Kusini imefanya. Tuliwatoa Tunisia katika mashindano na tulikuwa tayari kupambana na Morocco.

“Ikiwa utashinda hilo, basi kujiamini ni kukubwa sana na sasa ndoto zetu zote ziwe katika fainali.”

Kocha huyo Mbelgiji amekuwa na uzoefu mkubwa wa kutwaa taji la AFCON, akiwa na umri wa miaka 71 pale alipoiongoza Cameroon kutwaa taji la AFCON 2017.

Watatu familia wakatisha masomo kwa ujauzito
Aliyempasua mkewe tumbo, kuchemsha kichanga akamatwa