Neema Kenge (39) Mkazi wa Mtaa wa Mgonahazeru Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amejikuta njia panda baada ya watoto wake watatu kati ya 15 kukatishwa masomo kwa ujauzito, huku waliowafanya vitendo hivyo wakitoweka kusikojulikana.

Mmoja wa watoto Subira Simoni (19), ambaye ni Mtoto wa tatu katika familia ya mama Neema amesema alilazimika kukatisha masomo yake akiwa kidato cha pili, baada kurubuniwa na kupata ujauzito ambapo kwasasa ana mtoto mwenye umri wa miezi miwili na tayari ana ujauzito wa wiki mbili.

Katika hali ya kushangaza, Regina Simoni Mwenye umri wa miaka kumi na 17 na mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 nao wamejikuta wakikatisha masomo yao kwa kupatiwa ujauzito na kwa pamoja wameliomba jeshi la Polisi kuwakamata waliohusika kuwapa ujauzito na kutoweka lakini pia wakawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kutokana na changamoto wanazo kumbana nazo ikiwemo hali duni ya maisha.

Jirani wa Neema, Bea Joseph amesema Familia hiyo inakumbwa na changamoto nyingi kutokana na idadi kubwa ya watoto na hali duni ya maisha ya wazazi wao hivyo kama kuna mtu ataguswa asisite kutoa msaada.

Baada ya kupata taarifa kuhusu familia hiyo, Jeshi la Polisi Morogoro kupitia kwa Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Morogoro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pendo Mashurie alilazimika kufika, ili kuona namna ya kutoa msaada huku akikiri kuwepo kwa familia hiyo na kuahidi kuwatafuta waliohusika na kuwaomba wadau mbalimbali kutoa msaada, ili kuinusuru famila hiyo.

Neema ambaye ni mama wa nyumbani anajishughulisha na ufanyaji wa usafi katika nyumba za watu, ili aweze kupata kipato cha kuihudumia familia yake, huku mumewe akijushulisha na kazi ya ulinzi.

Shule zichapishe tozo kiwango cha karo - Serikali
Bafana Bafana wafikiria fainali – AFCON 2023