Wakazi wa Kitongoji cha Temekero C Mkoani Morogoro, wametakiwa kuwa na matendo mema, ili iwe mfano mzuri kwa Vijana chipukizi na hivyo kusaidia kuboresha maadili katika jamii.
Rai hiyo, imetolewa na Mkaguzi wa Polisi Dhikiri Pori ambaye pia ni Polisi Kata ya Kiroka Tarafa ya Mkuyuni, iliyopo Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Amesema, Vijana wamekuwa wakibadilika kwa kuona matendo ya kaka na wakubwa zao, hivyo uwepo wa matendo mema itakuwa imesafisha njia kwa wadogo zao.
Aidha, Mkaguzi pia alitoa elimu ya kupinga matumizi ya Dawa ya kulevya, usalama wao kwanza, kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na familia yangu haina muhalifu.