Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi sita, hatimaye staa wa zamani wa Manchester United, Jesse Lingard inaelezwa amefikia makubaliano ya kujiunga na FC Seoul ya Korea Kusini kwa mkataba wa miaka miwili.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Sky Sports, Lingard atasaini mkataba huo utakaokuwa na kipengele cha kumwezesha kuongezwa mwaka mmoja zaidi ikiwa ataonyesha kiwango bora.

Lingard ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kuachana na Nottingham Forest msimu uliopita, anatarajiwa kusafiri kwenda Korea kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho kabla hajaanza rasmi kuitumikia timu hiyo.

Mwezi uliopita Lingard alikuwa akihusishwa na Portland Timbers inayoshiriki Ligi Kuu Marekani lakini dili hilo lilifeli.

Kabla ya Portland alikuwa akifanya mazoezi na Etifaq ya Saudi Arabia ambayo inafundishwa na Steven Gerrard lakini hakusainishwa mkataba, licha ya kuangaliwa kwa muda mrefu.

Makala: Mauaji ya Binti kisa Bilauri ya Sharubati
Watoto 17,000 wadaiwa kuishi bila Wazazi