Imeripotiwa kuwa Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino alihitaji walau wachezaji watatu wapya kwenye kikosi chake wakati wa dirisha la usajili wa Januari.

Ikiwa ni dirisha lake la kwanza la usajili baada ya kutua Stamford Bridge, Pochettino alikabidhiwa majina ya wachezaji 12 wapya na wengine walihesabika kama mastaa wa siku za baadae.

Wakati timu hiyo ikishuhudia wachezaji 10 wa kikosi cha kwanza wakiondoka jumla, huku wengine wakitolewa kwa mkopo, kulikuwa na uwiano mzuri wa kikosi kuliko kilivyokuwa kipindi cha Graham Potter na Frank Lampard katika msimu wa 2022-23.

Hata hivyo, wachezaji sita waliosajili kwa ada inayozidi Pauni 30 milioni, Chelsea mambo yao ni magumu kwenye ligi msimu huu, timu ikishika nafasi za kati, hakuna tofauti na msimu uliopita.

Jambo hilo liliibua uvumi kwamba kocha Pochettino alihitaji sura mpya kwenye dirisha la Januari ili kwenda kubadili hali ya mambo kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.

Badala yake, Chelsea imeshindwa kusajili mchezaji yeyote mpya wa kuja kukiongeza nguvu kikosi cha kwanza, huku ikiwafungulia mlango wakali kama lan Maatsen na Armando Broja kwenda kwa mkopo Borussia Dortmund na Fulham.

Mshambuliaji wa kati ilionekana ni eneo ambalo Chelsea ilihitaji staa mpya, hasa baada ya kuonekana kuwa na mpango wa kumfungulia mlango wa kutokea Broja na Nicolas Jackson akiwa hana maajabu tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Villarreal na Christopher Nkunku amekuwa akisumbuliwa na majeruhi yanayomfanya ashindwe kuitumikia timu yake ipasavyo.

Na sasa, kocha Pochettino ataelekeza nguvu zake kwenye kumtumaini kinda wa Kibrazili, Deivid Washington.

Ajali ya moto: Waliotoa kibali ni watepetevu - Ruto
Radi yauwa wawili wakiangalia Luninga