Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Duniani – WFP, litaendeleza ushirikiano na Serikali Nchini ili kuhakikisha masuala ya menejimenti ya maafa yanaendelea kutekelezwa kwa tija na malengo yaliyokusudiwa, kwa kuimarisha uwezo wa kitaalamu kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi wa WFP, Brian John Bogart alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ofisi kwake jijini Dodoma.

Amesema, wataendelea kutoa ushirikiano hususani katika kuwajengea uwezo juu ya matumizi vifaa vya kiteknolojia ya kisasa ya kuchukua matukio na tarifa mbalimbali kwa kutumia vifaa aina ya Ndege Nyuki (drones) pamoja na kufadhili vifaa hivyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Jim Yonazi aliwashukuru WFP huku akisema Ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano hasa katika kipindi hiki cha mvua nyingi zenye kuleta maafa nchini kwa kuzingatia umuhimu wa taarifa na matukio hayo.

Watoto 17,000 wadaiwa kuishi bila Wazazi
Rais FKF akunwa na uwezo wa Taifa Stars