Latasha Harlins (15), alikuwa ni Binti wa Kiafrika ambaye aliishi jiji la Losd Angeles Nchini Marekani. Wakati fulani mwaka 1991 alishikwa na kiu hivyo angaikia duka la Vyakula na kuisogelea Bilauri ya Sharubati ili aweze kupoza koo kabla ya kuendelea na Pilika zake.

Wkati akishika Bilauri hiyo, ghafla alijikuta amesukumwa na kuanguka chini huku akimnyooshea mtutu wa Bunduki. Aliyemsukuma alikuwa ni Mwanamke mmoja mwenye asili ya Kikorea mke wa mmiliki wa Duka hilo la Vyakula aitwaye Soon Ja Du ambaye alidai Binti Latasha alitaka kumuibia fedha alizokuwa amehifadhi jirani na Bilauri ile ya Sharubati.

Taratibu Latasha aliamka na kurejesha Bilauri ile ya Sharubati mahala pake na kuanza kuondoka, lakini alipofika umbali wa hatua kadhaa, Jadu alimfyatulia risasi ya kichwa Binti Latasha na kumuua, halafu akaanza kupiga kelele kuomba msaada kwamba amevamiwa.

Asichokijua mfyatua risasi ni kwamba kulikuwa na mashuhuda wa tukio hilo mwanzo mpaka mwisho na pia Kamera ya ulinzi zilinasa tukio zima, hivyo taratibu zikafanyika na akafikishwa katika Baraza la usuluhishi la Mahakama ambalo lilimpata Ja du kuwa na hatia.

Siku ya hukumu, Baraza hilo likapendekeza Ja du afungwe kifungo cha miaka 16 jela, lakini Hakimu wa kesi hiyo aliamuru Ja du afungwe kifungo cha nje kwa kwa muda wa saa 400 pekee kulipa faini isiyopungua dola 500, akisema ingawa imethibitika kuwa Ja du alifanya mauaji hayo ya kinyama, lakini ilikuwa ni kwa ajili ya kujihami.

Hakimu alisema, katika kesi hiyo Latasha ni mtuhumiwa na angekuwa na kesi ya kujibu mbele za Mahakama endapo asingepoteza uhai wake, ilisikitisha sana na kuleta tafsiri ya ubaguzi wa rangi kwakuwa Latasha alikuwa ni mweusi kwani laiti angekuwa na ngozi ya mtu mweupe basi haki ingetendeka.

Hata hivyo, matokeo ya kesi ile yaliamsha maandamano makubwa jijini Los Angeles kwa watu weusi kutaka haki itendeke na hivyo kupelekea Wanaharakati kutumia jina la Latasha Harlins kudai haki dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani, kama sehemu ya kupigania usawa na utu.

Kouablan: Kwa Simba hii nitafunga sana
Jesse Lingard kutimkia mashariki ya mbali