Watu wawili, Juliana Robert (31) na Mateso Atanasi (35) wamefariki dunia kwa kupigwa na radi katika Kijiji cha Kigugu kilichopo Kata ya Sungaji, Tarafa ya Turiani, Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Taarifa ya Kamanda wa Polis Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama imeeleza kuwa, vifo hivyo vimetokea baada ya watu hao kupigwa na radi majira ya saa nane za usiku Februari 2, 2024 wakati wakiangalia Luninga ndani ya nyumba yao.
Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya Mvomero, kwa ajili ya kusubiri taratibu za mazishi huku Jeshi la Polisi la Polisi Mkoa wa Morogoro likitoa wito kwa Wananchi kuendelea kuchukua tahadhan kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limeeleza kuwa halii shwari na hii ni kutokana na jitihada zake kwa kushirikiana na Wananchi pamoja na vyombo vingine vya Ulinzi na usalama katika kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu.