Polisi Kata ya Sanu Baray iliyopo Mbulu Mkoani Manyara, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Sarmet amewataka Wananchi kuwa na hofu ya MUNGU na kuacha kushirikiana na watuhumiwa wa ukatili, kwani ni kinyume cha Sheria.
Sarmet ameyasema hayo wakati akitoa elimu ya kubaini na kutanzua uhalifu hususani ukatili wa kingono kwa watoto wadogo, katika mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji cha Sanu Baray na kuwataka kuwaona wahalifu kama adui asiyekubalika katika jamii na kuepukana nao.
Amesema, “Jeshi la Polisi lipo kusaidiana na jamii katika kulinda raia na Mali zao kwa mujibu wa Sheria, hamna budi Wananchi wote kuunga mkono jitihadi za kuhakikisha ulinzi na amani kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu vituo vya Polisi.”
Naye Mtendaji wa Kata hiyo – WEO, Agatha John amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kubuni mradi wa Polisi Kata, kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika kushughulikia na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, zikiwemo za kiusalama kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali