Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ wa Nigeria, Samuel Chukwueze amesema ana uhakika ‘Super Eagles’ itafanikiwa kuifunga Afrika Kusini katika muda wa kawaida.

Nigeria itacheza dhidi ya Afrika Kusini kesho Jumatano (Februari 07) katika mchezo wa Nusu Fainali ya Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ivory Coast.

Chukwueze amesema mchezo huo hautafika katika mikwaju ya Penati, kwania nakiamini kikosi chao kina uwezo wa kupata ushindi katika muda wa kawaida na kutinga Fainali itakayopigwa mwishoni mwa juma hili.

Winga huyo wa Klabu ya AC Milan pia ametupilia mbali dhana kwamba mlinda mlango wa Bafana Bafana, Ronwen Williams ni mtaalamu wa kuokoa Penati kabla ya Nigeria kumenyana na Afrika Kusini.

Kumbuka kwamba Williams aliweka jina lake kwenye vitabu vya historia kama kipa wa kwanza kuokoa Penati nne katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Cape Verde mwishoni mwa juma lililopita.

“Penati ni mchezo wa bahati, mtu yeyote anaweza kukosa. Ni ile ambayo [Williams] aliona kwamba aliokoa,” Chukwueze aliambia Toyin Ibitoye wa Hot Sport.

“Sisemi kuwa yeye si kipa mzuri, ni kipa mzuri, lakini jambo la muhimu zaidi ni sisi kushinda ndani ya dakika 90 au 120. Tutashinda bila kwenda kwenye Penati.

“Sio juu ya kuogopa, ni juu ya kuwa katika upande salama zaidi kwa sasa. Tumekuwa tukitazama Video za wapinzani wetu, ni wazuri lakini tutajaribu tuwezavyo na kushinda.”

Mashine mpya Man City 2024/25
Wabunge waridhia kuahirisha uchaguzi, Upinzani wapinga