Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City wamekubali kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Girona Sávio Moreira de Oliveira.

Imethibitika kukamilika kwa mazungumzo ya usajili wa Kinda hilo lenye umri wa miaka 19, baada ya mtaalam wa uhamisho wa Man City Fabrizio Romano kuandika katika ukurasa wake wa Mtandao wa X.

“Manchester City imekubali kumsajili Sávio kutoka kwa klabu ya Girona, dili hilo litakamilishwa mwishoni mwa msimu huu,” Romano ameandika.

“Hati za awali za uhamisho wa Savio zitatiwa saini katika siku chache zijazo.”

Amneongeza kuwa Mbrazil huyo ataendelea kucheza katika klabu ya Girona hadi mwisho wa msimu kabla ya kuondoka na kuelekea nchini England kujiunga na klabu yake mpya.

Kulingana na Romano, mabingwa hao wa Premier League walishinda mbio za kumsajili Kinda hilo licha ya ombi kutoka kwa vilabu vya Ujerumani na Uingereza.

Dabo ahimiza mabao zaidi Azam FC
Chukwueze – Hatutafika kwenye Penati