Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, Hugo Broos anaamini timu yake itafanya vizuri kwenye mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Nigeria ‘Super Eagles’.

Mtanange huo utakaopigwa Stade de la Paix, Bouake, ni Nusu Fainali ya kwanza ambayo itapigwa kuanzia saa 2:00 usiku kesho Jumatano (Februari 07).

Bafana Bafana walifanikiwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali baada ya kuishinda Cape Verde kwa mabao 2-1 kupitia Penati Jumamosi usiku ambapo kipa Rowen Williams aliokoa Penati nne na kuwa shujaa wa usiku huo.

Broos amasema kabla ya mchezo mkali dhidi ya Cape Verde kulikuwa na presha kubwa kwenye mchezo. Kila mtu alitaka kufuzu. Mchezo haukuwa kama ile iliyopita.

“Hatukuonesha utendaji sawa na tuliokuwa nao kwenye mechi zilizopita. Mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya Nigeria ambao wana wachezaji wazuri kama Lookman utakuwa tofauti. Hatuwezi kupoteza umakini. Wachezaji watakuwa katika hali nzuri,” amesema Broos.

Skudu: Nimejitafuta, nimejipata
Kutibu Tezi dume, Kisukari Bil. 346.42 kwa mwaka