Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema gharama ya kutibu wagonjwa wa sukari kwa mwaka ni Shilingi 300 bilioni na gharama za kutibu wagonjwa wote wa tezi dume ni Shilingi 46.42 bilioni.
Gharama hizo, zimepelekea jumla ya gharama za matibabu kwa magonjwa hayo mawili kufikia TZS bilioni 346.42 ambapo bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka ni Shilingi 200 bilioni.
Amesema, “ikitokea huduma ya matibabu kwa magonjwa haya mawili kutolewa bure, itapelekea huduma nyingine katika nchi kusimama.”