Serikali kupitia Wizara ya Maji, imesema inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji Mbesa-Ndaje utakaonufaisha vijiji vitatu vya Mbesa, Lijombo na Airport vilivyopo Tunduru kusini Mkoani Ruvuma, vyenye jumla ya wakazi 12,500.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ameyasema hayo hii leo Februari 6 2024 Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la mbunge wa Tunduru kusini ,aliyeuliza ni lini Mradi wa Maji wa Vijiji vya Mbesa, Lijombo na Airport utakamilika.

    Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi.

Akijibu swali hilo, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 40 ambapo ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo hadi kwenye tenki umbali wa Kilometa 13.45 umekamilika.

“Kazi zinazoendelea sasa ni pamoja na uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa Kilometa 32.132, ukarabati wa matenki mawili (2) yenye jumla ya ujazo wa lita 150,000, ujenzi wa tenki jipya lenye ujazo wa lita 50,000 na ujenzi wa vituo 25 vya kutolea huduma kwa wanachi Kazi zote hizo zinatarajiwa kukamilika Mwezi Agosti, 2024,” amesema.

Desabre: Tutakuwa mabingwa AFCON 2023
Kocha ahimiza mabaresho PSL