Johansen Buberwa – Kagera.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Mkoa Kagera, kwa kipindi cha Oktoba – Desemba, 2023 Takukuru Mkoa Kagera imefanikiwa kutembelea miradi 19 ya Maendeleo ya zaidi Bilioni 6.1 huku ikipokea jumla malalamiko 92 ambapo kati ya hayo 58 hayahusu rushwa na walalamikaji walielimishwa na kupewa ushauri.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Pilly Mwakasege ameyasema hayo hii leo February 6, 2024 wakati akizungumza na vyombo vya Habari na kuongeza kuwa, malalamiko mengina 34 yanahusishwa na vitendo vya rushwa ambapo uchunguzi wa majalada hayo yamefunguliwa na uchunguzi wa majalada 20 umekamilika na hatua stahiki zimechukuliwa, huku mengine 14 ya uchunguzi wake ukiwa bado unaendelea.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Pilly Mwakasege.

Amesema, TAKUKURU imekuwa ikipokea Malalamiko mengi yakihusishwa na vitendo vya rushwa kutokana na ongezeko la malalamiko ya madai baina ya wananchi na hivyo kushauriwa kufuata utaratibu wa sheria ya madai kwa mujibu wa Mikataba yao na kuzitaja Idara zinazolalamikiwa kuwa ni Halmashauri kwa jumla ya malalamiko 49 sekta binafsi 12 maji 3 ujenzi 9 Maliasili 7 Nishati 1 Uhamiaji 2 Polisi 4 Mahakama 3 uchukuzi 1 na Mamlaka ya Mapato 1.

Aidha, taasisi hiyo kwa mwaka huu wa 2024 Januari hadi Machi imejipanga kuelimisha umma kwa kwa kutumia njia mbalimbali ili kuongeza ushirikishwaji wa wananchi katika kuzuia vitendo vya rushwa, kutatua kero mbalimbali kwenye jamii kupitia Programu ya Takukuru Rafiki, kuendelea kufatilia matumizi ya rasilimali za umma kufuatia ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ili kuzuia fedha za umma pamoja na kufanya chambuzi za mifumo kwa lengo la kuzuia rushwa zinazosababisha na mapungufu yaliyopo kwenye mifumo ya utendaji wa sekta ya umma na binafsi.

Wanawake 10,829 wapatiwa vifaa vya kujifungulia
Hawamsaidii Rais kazi, wana makundi ya kuwasifia- Makonda