Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka taasisi ya Wakala wa vipimo Nchini kuendelea kusimamia vyema sheria, ili kumlinda mnunuaji na muuzaji wa bidhaa kuepuka uwizi unaoendelea.
Akizungumza hayo katika hafla ya uwekaji jiwe la Msingi katika jengo la wakala wa vipimo, iliyofanyika Jijini Dodoma, ambapo amesema mnunuaji na Muuzaji anapaswa kulindwa kama vigungu vya sheria vinavyo sema iwe serikali au sekta binafsi.
Amesema, “Wafanya biashara acheni mtindo wa kuchezesha mizani katika upimaji wenu, Na pia wekeni utaratibu mahususi kwenye upimaji wa rumbesa na vifungashio kwenye gunia,na nilazima wakala muhakikishe mnaondoa malalamiko ya wakulima wetu”. Amesema Majaliwa.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Ashatu Kijaji amesema Ujenzi wa Jengo hilo, unatarajia kumalizika Mwakani 2025 mwezi wa kwanza.
“Mpaka sasa ujenzi wa jengo hili umefikia asilimia 70 ambapo mwakani mwezi wa kwanza tutakuwa tumeshakamilisha ujenzi huu, kwaio ujenzi huu mpaka kumamilika kwakwe ni takribani miezi 30,” amesema.
Ujenzi wa jengo hilo ni utekelezaji na maelekezo ya Serikali kuwa na ofisi makao makuu ya Nchi Dodoma.