Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’, limetangaza tarehe ya ufunguzi Kombe la Dunia la mwaka 2026.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ametangaza kuwa ufunguzi wa fainali hizo utafanyika Juni 11, 2026.

Infantino ametaja uwanja utakaofungua michezo hiyo kuwa ni wa Azteca uliopo nchini Mexico itakapofanyika sherehe na mechi ya kwanza ya ufunguzi.

Uwanja wa Azteca unaobeba mashabiki elfu 83, ndipo ilipofanyika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1986 kati ya Argentina na England ambapo Diego Maradona alifunga goli maarufu la Mkono wa Mungu ‘Hand of God’.

Michuano hiyo itafanyika katika miji 16 iliyopo katika nchi tatu za Canada, Mexico na Marekani.

Fainali hizo zitahitimishwa Julai 19, 2026 katika Uwanja wa MetLife, New Jersey uliopo New York nchini Marekani.

Mudathir: Hatushuki kileleni
AFCON 2023 – Afrika Kusini ina deni kwa Nigeria