Serikali Nchini, imeanza majaribio ya mfumo wa ufundishaji mbashara ambao mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wa nchi nzima kwa wakati mmoja.
Mfumo huo ambao kwa sasa unafanyiwa majaribio kwa baadhi ya shule za Mikoa miwili ya Pwani na Dodoma, unamwezesha mwalimu kutoka kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa mikoa tofauti.
Utaratibu huo, pia unaleta tafsiri ya kwamba mbali na kurahisisha utendaji kazi, pia ni njia mojawapo ya kukabiliana na uhaba wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi shuleni.
Wakati Serikali inaendelea na majaribio ya mfumo huo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodom wamesema mfumo huo utawasaidia kupata uelewa kwa wepesi na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.