Beki wa timu ya taifa ýa lvory Coast, Max Gradel, amesema amekuwa akifananishwa na wachezaji waliowahi kufanya vizuri katika kikosi hicho.

Gradel amesema huenda msimu huu akawa ameonyesha kiwango bora lakini hana imani kama amewafikia wachezaji waliowahi kucheza katika timu hiyo.

Amesema wachezaji ambao huchaguliwa katika timu hiyo hucheza kwa ushirikiano mkubwa na kwa manufaa ya taifa zima.

“Nimekuwa nikifananishwa baadhi ya wachezaji kutokana na kiwango nilichoonesha, sawa kwangu, inanipa faraja na nitahakikisha naendelea kufanya vyema,” amesema.

“Ninaamini kila kizazi kina historia yake, ninafurahi kupata mrejesho mzuri wa kile ninachokifanya kwa manufaa ya taifa langu.”

Ivory Coast ambayo ndiyo wenyeji michuano ya AFCON, iliwahi kütwaa taji mwaka 1992 na 2015, na Jumapili (Februari 11) itacheza mchezo wa Fainali dhidi ya Nigeria kuwania Kombe la Ubingwa ‘AFCON 2023’.

Watuhumiwa utengenezaji Pombe feki wafikishwa Mahakamani
Jurrien Timber arudushwa kundini