Kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, inaelezwa ana mpango wa kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa sababu hajisikii furaha ya kuendelea kusalia kwenye viunga hivyo.

Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina ni mwaka mmoja tu tangu ajiunge na matajiri hao wa Jiji la London kwa ada ya Pauni 107 milioni na hivi karibuni alilazimika kufuta akaunti yake ya X baada ya kupokea meseji nyingi za kibaguzi na chuki kutoka kwa mashabiki waliochukizwa na kitendo cha timu hiyo kufungwa mabao 4-1 na Liverpool.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa na maisha magumu tangu ajiunge na Chelsea kwenye dirisha la majira ya baridi mwaka jana akitokea Benfica na mkataba wake wa sasa unatarajwa kumalizika mwaka 2031, huku msimu huu akicheza mechi 28 za michuano yote na kufunga mabao matano.

Sababu ya kuondoka inatajwa hafurahishwi na kinachoendelea ndani ya timu hiyo.

Ofori atajwa kuivurugia Black Stars
600 waomba kazi GFA