Hatma ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Msumbiji, Chiquinho Conde haitaamuliwa ndani ya miezi michache, wakati akiwa na mkataba hadi Julai, alisema Rais wa Shirikisho la Soka la Msumbiji, Feizal Sidat.

Vyombo vya habari vya Msumbiji viliripoti kuwa licha ya timu hiyo inayojulikana kama ‘The Mambas’ kutolewa mapema katika Kombe la Mataifa ya Afrika, lakini bado vichwa vyao viko juu baada ya kutoka sare dhidi ya Misri na Ghana.

Bado timu hiyo ilimaliza mkiani katika kundi lake baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoa kwa Cape Verde.

Sidat aliwaámbia waandishi wa habari kuwa kuna muda unahitajika kabla ya kuchukua uamuzi, huku akikiri kuwa kocha alifanya Vizuri katika mashindano hayo.

“Bila shaka yoyote kocha amefanya vizuri, nafikiri kutakuwa na mkataba unaopendekezwa kwa ajili yake…,” amesema.

Tangu alipoajiriwa mwezi Oktoba mwaka 2021, alipewa lengo la kuiwezesha timu hiyo kucheza Fainali za 34 za Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ivory Coast.

Lakini alikutana na vikwazo kibao wakati wa mchakato huo, ambako wachezaji waligoma hata kugomea mazoezi kwa sababu walikuwa wakidai malimbikizo ya fedha zao.

“Sitaki kuwa mnafiki. Kuna mambo yanahitaji kuboreshwa. Tuseme ukweli, kocha ndiye kiongozi katika chumba cha kubadilishia nguo, inabidi ajue kutawala chumba chake cha kubadilishia nguo, maana kocha wa taifa ndiye anayeita wachezaji. Kwa hiyo, ni juu yake kusema, rafiki zangu, hapa si mahali mnapaswa kugoma, mnapaswa kuzingatia mafunzo’. Mambo haya hayakusaidia taswira ya timu ya taifa,” aliongeza Sidat.

Msumbiji ina mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Somalia na Guinea katika mechi zijazo mwezi Juni.

Bei ya mwamba imefichwa Old Trafford
Ozil abembelezwa kurudi Ujerumani