Kocha Mkuu wa Vinara wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bayern Leverkusen, Xabi Alonso amesema kuwa hana mpango wa kujiunga na Liverpool kwa sasa kwa kuwa alipo ana furaha.

Alonso amekuwa akitajwa kuwa anaweza kujiunga na Liverpool baada ya Jurgen Klopp kutangaza kuwa ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kupata mafanikio ya kutosha.

Alonso ana rekodi nzuri kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ msimu huu akiwa hajapoteza mchezo wowote wa ligi ambao timu yake imecheza akiwa anaongoza Ligi Kuu Ujerumani kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya wababe Bayern Munich.

“Nilishtuka baada ya kusoma taarifa ya Klopp kuwa anaondoka, namheshimu sana Klopp, kwa sasa nina furaha hapa nilipo na ninafurahia kazi yangu, kila siku mambo yanazidi kubadilika. Nina maisha mazuri hapa Leverkusen.

“Kwa sasa naangalia mechi ijayo dhidi ya Bayern Munich ambayo ipo hivi karibuni, sidhani kama natakiwa kubaki sana kwenye kufikiri kuhusu Liverpool badala ya kuona ni jinsi gani tunaweza kufanya vizuri huku kwa kuwa ndipo maisha yangu yalipo kwa sasa,” alisema.

Leverkusen inaongoza ligi ikiwa na pointi 52 huku Bayern ikiwa nafasi ya pili na pointi 50 na timu hizo zinakutana kesho Jumamosi (Februiari 10) katika mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.

 

 

Tabora Utd kujitafuta kwa Namungo FC
Watendaji Kata waaswa kusimamia ulinzi, usalama Vijijini