Kocha Mkuu wa Tabora United, Goran Kopunovic amesema wanatarajia kujiuliza walikwama wapi hadi wakapoteza dhidi ya Simba SC, watakapowakabili Namungo keshokutwa Jumapili (Februari 11) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Tabora United wanashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 15 baada ya kucheza michezo 14 wakiwa wameshinda mechi tatu, sare sita na kufungwa mechi tano.
Wakati Namungo wako nafasi ya nane wakiwa na pointi 17 katika mechi 14 wakishinda mechi tano, sare tano na kupoteza michezo mitano.
Kopunovic amesema mchezo uliopita walifanya makosa mengi hasa kwenye eneo la ulinzi, lakini wameyafanyia kazi ili yasijirudie watakapowavaa Namungo.
Tunahitaji matokeo ya ushindi katika mchezo huu japokuwa halitakuwa jambo rahisi licha ya kuwa tutakuwa nyumbani kwani wapinzani wetu wako kwenye nafasi nzuri kuliko sisi, hivyo watahitaji kupambana kutafuta pointi kwetu.
Timu yangu inapaswa kupambana ili kuondoa makosa ya mchezo uliopita, timu ipo kwa ajili ya kutafuta pointi tatu, najua itakuwa ngumu tutakuwa nyumbani lakini kwa jinsi tulivyojiandaa naamini tutaibuka na ushindi,” amesema Kopunovic.