Boniface Gideon –  Mkinga.

Wavuvi na Wajasiriamali pamoja na wanachama wa vikundi vya utunzaji wa mazingira Kata ya Boma wilayani Mkinga mkoani Tanga wamenufaika na mradi wa mfuko wa kutunza Bahari (MKUBA) unaosimamiwa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network, Mradi huo unafadhiriwa na Jumuiya ya umoja wa nchi za NORAD.

Wakazi hao wamenufaika kwakupatiwa Elimu ya utunzaji wa mazingira,usimamizi Bora wa rasilimali Bahari pamoja na usimamizi Bora wa fedha nakupatiwa shilingi mil.10.5 kwaajiri yakusaidia mitaji kwa wanachama wa vikundi vya watunzaji Bahari.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla yakukabidhi fedha kwa vikundi 5 vya Boma,Mratibu wa Mradi huo mkoa wa Tanga kutoka Shirika la Mwambao Coastal Community Network Ahmed Salim, alisema Mradi huo unalenga kupunguza shughuli za kibinadamu Baharini ili kupunguza uharibifu kwa Wilaya zilizozungukwa na Bahari ,Pangani,Muheza ‘Kigombe’, Tanga jiji na Mkinga.

Alisema jitihada za ziada zinahitajika nakwamba moja Kati ya uharibifu mkubwa Baharini ni Uharibifu wa matumbawe ambayo ndio makazi ya Samaki kwaajili yakuzariana, ukataji wa miti ya mikoko,utupaji wa taka ngumu zinazoperekea viumbe Bahari kufa pamoja na uvuvi haramu,

“Huko Baharini hali sio nzuri, Kuna uharibifu mkubwa wa Mazingira,hivyo kama hatutachukua hatua madhubuti hali itakuwa mbaya zaidi huko mbeleni, hivyo niwaombe wananchi kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake,tuhakikishe fukwe zinakuwa Safi muda wote,upandaji miti aina ya mikoko utasaidia kurudisha uhai wa viumbe Bahari,” alisema Ahmed

Kwa upande wake katibu tawala Wilaya ya Mkinga ,Palango Abdul aliwataka wanufaika wa fedha hizo pamoja na Elimu ya Mazingira na usimamizi Bora wa rasilimali Bahari pamoja na fedha kutumia vyema fursa hiyo,

Alisema “Halmashauri ya Wilaya hiyo imewekeza nguvu nyingi katika kuhakikisha Bahari na viumbe vyake vinaendelea kuwa salama kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae lakini baadhi ya watu huwa wanafanya uharibifu makusudi, “Kuna watu wanafanya uharibifu makusudi ,niwaambie tu kuwa Serikali ipo macho muda wote,mtu yeyote atakayefanya uharibifu Baharini atachukuliwa hatua za kisheria kama mharifu mwengine tu.”

 

Rais Samia kuongoza mazishi ya Lowassa
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi: Majaji wapewa uhakika