Wakati tetesi za kuondoka kwake zikiwa zinazidi kupamba moto, Mabosi wa Paris St Germain wanadaiwa kumpa mkataba mpya wa miaka miwili Mshambuliaji wao Kylian Mbappe ikiwa ni sehemu ya kumzuia asiondoke dirisha lijalo na anahusishwa kujiunga Real Madrid.

Mkataba huo mpya unadaiwa kuwa na thamani ya Pauni 136 milioni ambazo ni mjumuisho wa pesa atakazopata Mbappe kutokana na mshahara na bonasi ya Usajili.

Kupitia tovuti ya AS, inaelezwa Mbappe mwenye umri wa miaka 25, ameshafanya uamuzi wa kuondoka PSG mwisho wa msimu na kutua Madrid, lakini mabosi wa PSG hawataki kukubaliana na hilo.

Mkataba wa sasa wa Mbappe unamalizika mwisho wa msimu huu na alihusishwa kuondoka tangu mwanzo wa msimu lakini ilishindikana.

Staa huyu mara kadhaa katika kipindi cha hivi karibuni amekuwa akihusishwa na Liverpool ingawa inaonekana kuwa ngumu kutua huko kwa sababu ya ndoto yake ya kuichezea Real Madrid.

Uhaini: Serikali kuwarejeshea adhabu ya kifo waasi
Hali hii isipokabiliwa kuna madhara makubwa - Zito