Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland amethibitisha timu yake haiwezi tena kushinda mataji matatu kwa msimu huu.

Haaland ambaye alifunga mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Everton Man City ikishinda mabao 2-0, amefikisha mabao 52 kwenye mechi 53 za Ligi Kuu England alizocheza tangu aanze kucheza ligi hiyo.

Mabao hayo mawili amefunga kwa mara ya kwanza tangu aliporejea baada ya kuwa nje kwa majeraha tangu Novemba mwaka jana.

Haaland haamini kama timu hiyo inaweza kuchukua mataji matatu kama ilivyokuwa msimu uliopita kwa sababu ya ushindani uliopo kwa sasa kwenye mashindano mbalimbali.

Kwenye Ligi Kuu England mshindani wao wa karibu anaonekana ni Liverpool ambayo kwa sasa inaongoza kwa tofauti ya Pointi mbili lakini Man City ina faida ya mechi moja zaidi.

Kwenye Ligi ya Mabingwa ipo hatua ya l6 bora na itacheza dhidi ya Coppenghagen ya Denmark na FA ipo raundi yanne na itakutana na Luton Town.

Ingawa nafasi bado ipo lakini Haaland anaamini kutakuwa na kazi kubwa ya kufanya ili kufanikisha hilo.

“Hapana hatuwezi kufanya hivyo.” alisema Haaland alipoulizwa.

“Watu wanajaribu kutaka kutuzuia lakini tuna timu nzuri na sasa tumefanikiwa kushinda mechi ya 10 mfululizo.”

Wakati nina majeraha kilikuwa ni kipindi kigumu, lakini kilinifanya akili yangu ifikirie tofauti kidogo.”

Baada ya mchezo huo Man City itakuwa na kibarua mbele ya Coppenhagen kwenye Ligi ya Mabingwa ugenini kabla ya kurudi na kuvaana na Chelsea Februari 17.

Rais Samia zungumza na Papa Francis Vatican
Majibu ya Mzazi yamshangaza Polisi, achukua hatua