Kiungo kutoka nchini Uholanzi Frenkie De Jong anazidi kukatishwa tamaa na maisha ya FC Barcelona na Chelsea inaweza kumpa njia ya kuondoka kwa dau la uhamisho wa euro milioni 100 msimu wa majira ya joto, kwa mujibu wa ESPN.

Muda wa Mholanzi huyo akiwa pale Katalunya unakabiliwa na nia ya kutaka huduma yake kutoka kwa timu kama Manchester United, ingawa sasa yuko katika msimu wake wa tano na Bařca tangu asajiliwe kutoka Ajax mwaka 2019 kwa euro milioni 75.

De Jong siku zote amekuwa akitaka kubaki na wababe hao wa La Liga licha ya nia ya Barca kumuuza katika miaka ya hivi karibuni, lakini ESPN inasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuondoka msimu wa majira ya joto.

Kiungo huyo anasemekana kusikitishwa na kiwango cha ,Blaugrana hao kwenye LaLiga, huku wakipokea kichapo kwenye Supercopa de Espana na Copa del Rey.

Kocha Xavi tayari amethibitisha kuwa atajiuzulu nafasi yake mwishoni mwa msimu huu.

ESPN imeongeza kuwa Mkurugenzi wa Michezo, Deco amejaribu kujadili tena kuongeza mkataba wa De Jong hadi mwaka 2029, lakini hadi sasa imekuwa haiwezekani’ kufikia makubaliano.

Inadaiwa kuwa Chelsea ya Mauricio Pochettino itakuwa tayari kutumia euro milioni 100 kumsajili De Jong, ikiwa tayari Enzo Fernandez, Moises Caicedo na Romeo Lavia wamegharimu kiasi kikubwa cha fedha.

‘The Blues’ walifanya vibaya katika dirisha la usajili la Januari na wanasemekana kuhofia kukatwa pointi iwapo watamtimua Pochettino na wafanyakazi wake, ikizingatiwa kuwa wanaweza kukiuka kanuni za Faida na Uendelevu (PSR).

Man Utd bado walikuwa na nia ya kumnunua De Jong msimu uliopita wa majira ya joto, huku Bayern Munich na Paris Saint-Germain zilitajwa pia.

Philips afichua maisha Man City
Beki DR Congo achekelea kuifunga Misri