Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC inakusudia kurejesha adhabu ya kifo ambayo iliisitishwa miaka 20 iliyopita, kwa wanajeshi wanaopatikana na hatia ya uhaini dhidi ya waasi wa M23, kulingana na ripoti ya baraza la mawaziri.

Hatua hiyo inatokana na Waziri wa sheria kuwasilisha barua kwa Baraza la Mawaziri kuhusu kuondoa katazo la hukumu ya kifo kwa Wanajeshi.

Msemaji wa Serikali ya DRC, Patrick Muyaya amesema hukumu za kifo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na Mahakama nchini humo, lakini zilibadilishwa kuwa za kifungo cha maisha gerezani tangu kuondolewa kwa hukumu ya kifo mwaka wa 2003.

Alisema, “Katika lengo la kukomesha uhaini, Baraza la ulinzi lilimuomba Rais kuondoa katazo hilo kipindi hiki ambapo, nchi inakabiliwa na uchokozi kutoka Rwanda, ambayo inakanusha madai ya kuwasaidia waasi wa M23.”

Majibu ya Mzazi yamshangaza Polisi, achukua hatua
Mabosi PSG wampa mkataba Mbappe