Scolastica Msewa – Saadani.

Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Saadani, Simon Aweda amewataka Wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi za Taifa kulima mazao ambayo ni chukizo kwa Tembo na kufuga nyuki, ili kumsaidia kudhibiti wanyama hao kuingia katika makazi na mashamba yao wasifanye uharibifu.

Aweda ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Saadani Chalinze Mkoani Pwani, kuhusu kujibu malalamiko ya Wananchi wa Maeneo ya Kiwangwa ya uwepo wa matukio ya mara kwa mara ya Tembo kuvamia mashamba na makazi ya Wananchi jambo ambalo ni hatari.

Amemesema mazao ambayo Tembo hawayapendi ni pamoja na Pilipili, zao la Alzeti, ufungaji wa Nyuki kwa kuweka mizinga kuzunguka maeneo ya mashamba na makazi yao.

“Mizinga ya nyuki kwa kuweka pembezoni ikiwa na nyuki husaidia kufukuza tembo wasiingie kwenye mashamba na makazi ya watu na pia Kuna mbinu ya kutengeneza tofali za Kuchanganya na pilipili na mavi ya tembo ukichoma moto tofali hizo ndani ya maeneo yako husaidia kufukuza tembo na kudhibiti uharibifu huo unaweza kusababishwa na wanyama poli hao” amesema Aweda.

Amesema, Hifadhi za Taifa na Wanyama waliomo ni mali ya Wananchi na jukumu la TANAPA ni kulinda ili kuhifadhi raslimali hizo ziendelee kuingizia taifa mapato hivyo Wananchi wanawajibu wa kuhakikisha usalama wa wanyama poli hao na kudai kuwa Tembo hawapendi kelele hivyo Wananchi wakiwaona tembo watumie mbinu ya kupiga madebe wakiwa mbali kuwafukuza mashambani na kwenye makazi yao.

Mlipuko wa bomu wauwa watatu, maelfu wakimbia makazi yao
Broos: Nilitamani kuacha kazi Bafana Bafana