Klabu ya Aston Villa, itakosa kwa muda huduma ya kiungo, Boubacar Kamara, baada ya kupata majeraha ya goti.

Kamara mwenye umri wa miaka 24, alipata majeraha ya goti juzi Jumatatu (Februari 12) wakati timu yake ikipoteza mabao 2-1, katika mchezo dhidi ya Manchester United.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa klabu hiyo, ilieleza kuwa, Kamara alipelekwa hospitali kufanyivwa vipimo kwa lengo la kujua ukubwa wa jeraha alilopata.

Imeelezwa kuwa, baada kufanyiwa vipimo, taarifa rasmi ya maendeleo yake itatolewa na kujulikana atakaa nje ya dimba kwa muda gani.

Raia huyo wa Ufaransa, tayari ameshacheza mechi 30 katika kikosi cha Aston Villa, msimu huu 2023/24.

Pia, amefunga bao moja katika michuano ya Kombe la Ligi na kutoa pasi ya moja ya mwisho ya michuano ya Ligi Kuu ya England msimu huu 2023/24.

“Kamara hatakuwepo kikosini katika baadhi ya mechi baada ya kupata majeraha ya goti, tayari ameshapelekwa hospitali kufanyiwa vipimo kujua ukubwa wa tatizo alilonalo,” imesema taarifa hiyo.

Villa imewakosa baadhi ya wachezaji wakiwemo Kiungo raia wa Argentina, Emi Buendia na beki wa kati, raia wa England Tyrone Mings kutokana na majeraha ya muda mrefu ya goti wakati beki Ezri Konsa pia anauguza jeraha la goti.

Simba SC yahamia Jamhuri Morogoro
Dawati la jinsia lainusuru familia ya Watoto 15 Moro