Mwanzoni mwa mwezi Januari 2024 Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Morogoro chini ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Pendo Meshurie walibaini familia ya mama mmoja aliejulikana kwa jina la Neema Kenge (39) mwenye watoto 15.
Alikuwa akiishi nao kwenye mazingira magumu kutokana na hali duni ya maisha aliyonayo huku Mume wake akifanya kazi ya Ulinzi kwenye Nyumba za watu. Familia hii inaishi katika mtaa wa Mgonanzeru uliopo Manispaa ya Morogoro.
Mara baada ya kuibua jambo hilo, Mkaguzi Meshurie kwa kushirikiana na Askari wa Ofisi yake, walianza kutafuta wadau mbalimbali kwaajili ya kuisaidia familia hiyo.
Kufikia Februari 13, 2024 tayari walishapatikana wadau kadhaa kwaajili ya kuwalea na kuwasomesha watoto wote wanaendelea na masomo wakiwemo watatu wakike waliokatisha masomo yao kutokana na kupata ujauzito.
Meshurie amesema, mbali na kupata wadau hao kama dawati wamejichanga na kupata vitu mbalimbali vya kuwasaidia ikiwemo nguo, madaftari mabegi pamoja na vitu vingine.