Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa umeme kwenye gridi ya Taifa (Gridi imara), ili kuwezesha wananchi kupata huduma hiyo muhimu ya umeme kila sehemu ya Nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula aliyejibu swali bungeni kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

Swali hilo la msingi limeulizwa na Mbunge wa Kyela, Ally Jumbe ambaye alitaka kujua Ujenzi wa Kituo cha kupoza Umeme cha Kyela utaanza lini, ambapo Kitandula alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. Bilioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kyela mkoani Mbeya ili kuweza kuboresha huduma ya umeme wa uhakika kwa wananchi.

Aidha, aliongeza kuwa maandalizi ya awali kuhusu utekelezaji wa mradi huo yanaendelea ikiwemo upembuzi yakinifu na tathimini ya athari ya mazingira kwa ajili ya kujua gharama halisi ya ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme.

“Kazi hizo za maandalizi zinatarijiwa kukamilika mwaka wa fedha 2024/2025 na utekelezaji wa mradi huo utaanza mara baada ya kupatikana kwa fedha,” alisema Kitandula.

Kwaresma: Kilaini atoa darasa upataji huruma ya Mungu
Bosi wa Mayele amuombea msamaha Young Africans