Klabu za Newcastle United na Arsenal zote za England zimeanza kujipanga baada ya kusikia taarifa kwamba Brentford inamfuatilia Mshambuliaji kutoka nchini Canada na Klabu ya wa Lille ya Ufaransa Jonathan David, 24, kama mbadala wa lvan Toney ambaye huenda akaondoka katika dirisha la majira ya kiangazi.

Brentford imejaribu kufanya mazungumzo na Toney ya kusaini mkataba mpya lakini hayajafanikiwa na hivyo inatafuta mbadala wake.

Toney mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo 2025 na kutokana na kiwango chake tangu kuanza kwa msimu huu amezivutia timu nyingi, huku Newcastle na Arsenal zikijiandaa kuwasilisha ofa ya kumnunua.

Brentford inataka kufanya biashara nzuri mwisho wa msimu katika dirisha la kiangazi ili kutoruhusu kuondoka bure mwishoni mwa mkataba wake ikaambulia hasara.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote.

Mexime: Kazini kwangu bado kuna kazi
Kwaresma: Kilaini atoa darasa upataji huruma ya Mungu