Kinda wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Simon Adingra amesema mchezo wa Fainali dhidi ya Nigeria ulikuwa moja ya mechi bora kwenye maisha yake ya soka.

Adingra mwenye umri wa miaka 22 alitoa pasi zilizozaa mabao yote mawili kwenye mchezo huo na kuzawadiwa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo.

Adingra alikuwa hazuiliki kwa ukokotaji, chenga za maudhi na krosi ambazo ziliwapa wakati mgumu mabeki wa Nigeria wakati wote wa mhezo huo.

Chipukizi huyo amesifu mchango wa wachezaji wenzake kwenye mafanikio hayo ya kushinda ubingwa wao wa tatu wa michuano hiyo.

“Tulicheza kwa umoja, sisi ni mabingwa wa Afrika na ni kitu kizuri. Nimeshuhudia moja ya nyakati bora kwenye maisha yangu na hiyo ni kutokana na juhudi za kila mmoja kwenye timu,” amesema Adingra.

Tabora Utd wafichua kinachoendelea kambini
Bafana Bafana yapongezwa Afrika Kusini