Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi (TPLB) imezitoa hatiani klabu ya Simba SC na Young Africans kwa makosa ya kujihusisha na Ushirikina michezoni.

Kamati hiyo ilikutana juzi Jumanne (Februari 14) kwa ajili ya kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi kadhaa ambayo yameambatana na adhabu kwa wachezaji na klabu zao.

Simba SC imekutwa na ahtia ya kujihusisha na Ushirikiana wakati akiwa katika maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tabora United uliopigwa mjini Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mapema mwezi huu.

Taarifa ya Kamati hiyo ya TPLB imeeleza kuwa, Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh 1,000,000 (Milioni Moja) kwa kosa la Mashabiki wake ambapo wametambuliwa kwa msaada wa picha jongeo (video) zilizosambaa mtandaoni kuonekana wakimwaga vitu vyenye asili ya unga katika uwanja wa Alli Hassan Mwinyi wakati wachezaji wa klabu hiyo wakijiandaa kuanza mazoezi.

Tukio hilo ambalo lilifanyika siku moja kabla ya mchezo huo uliomalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa 4-0, limetafsiriwa kama vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina jambo ambalo ni kinyune na matakwa ya Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa klabu.

Kwa upande wa Young Africans Mchezaji Kibwana Shomari wa klabu ya Young Africans ametazwa faini ya Sh. 1,000,000 (Milioni Moja) kwa kosa la kuonekana akiondoa taulo la mlinda mlango wa klabu ya Mashujaa lililokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea, jambo liiloashiria imani za kishirikina

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Naye Mchezaji Clement Mzize wa klabu ya Young Africans ametozwa faini ya Shilingi 1000,000 (Milioni Moja) kwa kosa kuonekana akiondoa taulo la Mlinda Lango wa Klabu ya Dodoma jiji lililokuwa limewekwa kwenye lango la klabu hiyo wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya45 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa wachezaji.

Wakati huo huo Klabu ya Mashujaa imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (Milioni Moja) kwa kosa la mashabiki wake wanne (4) kuonekana wakiingia kwenye chumba cha kuvalia cha klabu hiyo kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:50 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mohamed Salah amerudi kazini
Tabora Utd wafichua kinachoendelea kambini