Serikali Nchini, imesema kuwa imefanya tathmini ya vituo vya afya vikongwe vinavyohitaji ukarabati. Hadi kufikia mwaka 2023 jumla ya vituo vya afya 202 chakavu vimeainishwa kote nchini kikiwemo kituo cha Afya Galapo ambapo vitatengewa bajeti kwa ajili ya ukarabati kwa awamu.

 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo aliyeuliza lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Galapo – Babati.

Akijibu swali hilo Dugange amesema Serikali inaendelea kuona uwezekano wa kutenga bajeti kupitia programu ya Banki ya Dunia kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha afya Galapo.

Watatu wasimamishwa kazi kwa utoro, wawili kikaangoni
Kura ya kuahirisha uchaguzi yafutwa Senegal