Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kassim ‘Kiduku’ amemtaka Hassan Mwakinyo kumaliza utata kati yao kwa kukubali kupanda ulingoni.
Akizungumza na Dar24 Media mjini Morogoro, Bondia huyo amesema amechoka kusikia vijembe vya mara kwa mara, sasa ni vyema wakapanda ulingoni ili kumaliza utata.
Mashabiki zetu wana imani kubwa na sisi lakini ili kumaliza haya maneno na tambo za mtaani lazima tupande ulingoni, Mwakinyo kama anataka kuwaaminisha mashabiki zake kuwa ni zaidi yangu aje asaini niko tayari,” amesema Kiduku.
Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mchezo wa ngumi nchini, mara kadhaa Mwakinyo ameomba mapromota kujitokeza ili kuandaa pambano hilo, lakini mpaka sasa hakuna aliyejitokeza.
Hata hivyo, hivi karibuni Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) ilisema Mwakinyo na Kiduku ni mabondia wanaocheza uzito tofauti, ni ngumu kucheza lakini inawezekana kama mmoja atapunguza au kuongeza uzito ii kuwa sawa.
Twaha anacheza Super Middle Kilo 76 wakati Mwakinyo anacheza Super Welter Kilo 69.