Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema kuondoka kwa baadhi ya wachezaji kwenye kikosi chake hakutaathiri mwenendo wa timu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Nyota sita wa timu hiyo akiwamo Shiza Kichuya, Hassan Maulid, Hassan Kapalata, Edward Maka, David Bryason na Wema Sadock wanatarajiwa kwenda katika nafunzo ya kijeshi kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kocha huyo amesema kikosi chake kina idadi kubwa ya wachezaji wa kuziba nafasi za nyota hao hivyo hadhani kama wanaweza kutetereka katika kipindi hicho.

“Tuna kikosi kipana na tulijandaa na hilo ndio maana sina wasiwasi nina imani na wachezaji waliopo na ninaamini hatutotetereka,” amesema Malale.

Kocha huyo amekiri kwamba wachezaji hao wana mchango mkubwa kwenye kikosi chake lakini lazima awaruhusu kwenda mafunzoni kwa ajili ya maisha yao ya baadae.

Amesema wataendelea kupambana na anatarajia watakaporudi watakuwa na mchango mkubwa katika kuifanya JKT Tanzania kumaliza msimu kwenye malengo yake.

Ndani ya miezi mitatu timu hiyo itakua na kibarua cha kuzisaka pointi tatu dhidi ya Young Africans, KMC FC, Kagera Sugar, Mashujaa, Tanzania Prisons, Tabora United, Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar.

Taifa Stars yaruka kihunzi AFCON 2025
Kobbie Mainoo apigiwa chepuo Euro 2024