Mahakama ya Mombasa imefahamishwa kuwa Mhubiri tata Paul Mackenzie na wafuasi wake, wamekuwa wakisusia kula kwa siku zisizojulikana.

Wakili wa Mackenzie na wafuasi wake,  Wycliffe Makasembo ameiambia Mahakama kwamba washukiwa hao wamesusia kula, kwa madai kwamba wamekuwa wakiteswa na Serikali tangu kukamatwa kwao.

Hii leo Februari 20, 2024 baadhi ya wafuasi hao wameshindwa kushuka kwenye magari ya Polisi hali iliyolazimu kuwapa usaidizi na wengi wao wakionekana kudhoofika kiafya, na wengine pia kushindwa kufika kizimbani kusikiliza kesi yao.

Dhumuni la kufikishwa Mahakamani hapo lilikuwa ni kusikiliza shauri iwapo watapatiwa dhamana au la, ambapo Hakimu wa Mahakama ya Mombasa alitoa amri kuwa Wakili upande wa utetezi aweze kusikiliza shauri hilo kwa niaba yao.

Source: Bahari FM.

Dkt. Biteko ataka Miradi ya Umeme Jotoardhi iendelezwe
Chelsea kutumia udhaifu FC Bayern Munich