Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linachunguza tukio la Mtu mmoja anayedaiwa kujifanya Mganga wa kienyeji na kuwapa dawa iliyowalewesha Watu 16 wa Familia moja, kisha kuwaibia simu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jumanne Muliro  imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 18, 2024 huko mji mwema Kigamboni, majira ya saa tatu usiku.

Mtu huyo alifika nyumbani kwa Familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibu Fatuma Abdalla (52), aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu na kisha kuwanywesha dawa iliyowalewesha na walipopoteza fahamu aliwaibia simu tani za mkononi.

Amesema, “kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamtafuta Mganga huyo lakini limemkamata kwa mahojiano Mtu mmoja aitwae Jalala Ally Said anayedaiwa kushirikiana na Mganga huyo.”

Kuhusu Wagojwa walioleweshwa, Muliro amesema wao walilazwa na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni na 13 kati yao walisharuhusiwa huku watatu wakiendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Mbappe aandaliwa jezi namba 10
Suarez: Nilivuruga dili la Benzema kusajiliwa Arsenal