Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, amemuomba radhi Kalvin Phillips kwa kusema kuwa kiungo huyo alikuwa na uzito mkubwa aliporejea kutoka Kombe la Dunia la 2022.
Guardiola aliwaambia waandishi wa habari kwamba Phillips hakuwa katika hali nzuri ya kufanya mazoezi baada ya kurejea kutoka Qatar, ambako alitumiwa kwa dakika 40 pekee katika mechi mbili za akiba kwenye kikosi cha England.
Phillips alivumilia wakati mgumu akiwa City baada ya kusajiliwa kutoka Leeds United mnamo 2022, alianza mechi sita pekee ndani ya miezi 18, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka miaka 28, alijiunga na West Ham United kwa mkopo mwezi uliopita.
Baada ya kuhamia West Ham, kiungo huyo alisema kujiamini kwake kumepata “pigo kubwa” kutokana na matamshi ya Guardiola.
“Ndiyo, samahani,” alisema Guardiola akiwaambia waandishi wa habari kuhusu kumuomba radhi Phillips
“Ninaomba msamaha kwake. Nilizungumza naye kabla ya kutoa maoni. Sijawahi, huwa sizungumzi na timu kabla sijasema kitu hapa, au mchezaji katika kesi hiyo.”
City, ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, na tayari wamepunguza pengo la alama dhidi ya Liverpool inayoongoza kwa tofauti ya alama moja baada ya kushinda dhidi ya Brentford usiku wa kuamkia leo Jumatano (Februari 21).