Ni Rasmi Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich Thomas Tuchel ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu 2023/24.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 alichukua nafasi ya Julian Nagelsmann aliyeondolewa klabuni hapo mwezi Machi 2023, na alikuwa na mkataba hadi Juni 2025.

Hata hivyo Tuchel anaendelea kuheshimiwa klabuni hapo kufuatia kuiwezesha FC Bayern Munich kutwaa Ubingwa wa Ujerumani msimu uliopita, licha ya msimu huu mambo kumuendea kombo, hali iliyopelekewa kusitishiwa mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen amesema pande zote mbili zimekubaliana kuvunja Mkataba, na wamemtakia kila la kheri katika kipindi hiki cha kumalizia sehemu ya kazi yake klabuni hapo.

“Ushirikiano wetu na Kocha Tuchel umefikia kikomo, tutakuwa naye hapa hadi mwishoni mwa msimu huu, tumefanya mazungumzo ya wazi kati yetu kama viongozi na upande wake, tunashukuru tumekubalianiana vizuri.”

“Lengo letu ni kufanya maelewano ya kimichezo na kocha mpya kwa msimu wa 2024-25,” ameongeza.

“Hadi wakati huo, kila mtu katika klabu ana changamoto kubwa ya kufikia kiwango cha juu iwezekanavyo katika Ligi ya Mabingwa na Bundesliga.

“Pia ninawajibisha timu kwa uwazi. Hasa katika Ligi ya Mabingwa, tuna hakika baada ya kushindwa dhidi ya SS Lazio, tutatinga Robo Fainali huku mashabiki wetu wakiwa nyuma yetu.”

Kwa sasa kikosi cha Tuchel kipo nyuma kwa tofauti ya alama nane dhidi vinara wa msimamo wa Ligi ya Ujerumani Bayer Leverkusen, kufuatia kupigwa katika michezo mitafu mfululizo

Kipigi kikubwa miongoni mwa vipigo hivyo ni dhidi ya Leverkusen iliyochomoza na ushindi wa 3-0, kicha walichapwa na SS Lazia 1-0 katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.

Mwishoni mwa juma lililopita Bayern ilikubali kichapo kingine kutoka kwa Buchum kwa kufungwa 3-2.

Twiga Stars mguu sawa Dar es salaam
Kisa mauaji: Wananchi wafunga barabara Babati